RAS Mara atembelea MJNUAT
RAS Mara atembelea MJNUAT
01st Jan, 1970

Katibu Tawala Mkoa wa Mara Bw. Gerald Kusaya jana tarehe 14/05/2024 amefanya ziara yake ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT) kilichopo Butiama.

Katika ziara hiyo, Bw. Kusaya amekagua miradi ya ujenzi katika Kampasi Kuu Butiama na Kampasi ya Oswald Mang’ombe ambayo inatekelezwa na chuo.

Katibu Tawala Kusaya amesema ametembelea Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia ili kujionea miradi inayotekelezwa na kuonyesha kufurahishwa na hatua za ujenzi zilizofikiwa.

Kwa kuzingatia kuwa, chuo kina maeneo katika wilaya mbalimbali, Bw. Kusaya amekiagiza chuo kihakikishe kinalinda maeneo hayo.

“Haya maeneo (ya chuo) tuliyonayo ni vizuri sasa tukayalinda. Kwa kutumia wataalmu tulionao tunaweza tukatengeneza kitu kinachoweza kujua alama za mipaka ya maeneo yetu kama nguzo ndefu zenye rangi,” amesesisitiza Bw. Kusaya.

Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia kinatekeleza ujenzi wa Kampasi Kuu Butiama chini ya Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) na Mradi wa Ukarabati na Ujenzi katika Kampasi ya Oswald Mang’ombe. mradi unaofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.